Queens yaibuka mshindi mbele ya Baobab

Kikosi chetu cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Baobab Queens katika mchezo wa Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League SLWPL uliofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Kinara Jentrix Shikangwa alitupatia bao la kwanza dakika ya 23 baada ya kumalizia mpira akiwa nje ya 18 akiwaacha walinzi wa Baobab wakiwa hawana la kufanya.

Nahodha Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata majeraha dakika ya 29 nafasi yake ikachukuliwa na Zainabu Mohamed.

Kiungo Joelle Bukuru alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la pili kwa shuti kali nje ya 18 dakika ya 82 lililotuhakikishia ushindi huo wa ugenini.

Kocha Mkuu Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Vivian Corazone, Wema Richard na Mwanahamisi na kuwaingiza Zainabu, Dhanai Bhobho, Asha Mwalala na Esther Mayala.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER