Queens yafanya mazoezi ya mwisho kujiwinda na Green Buffalos

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Annex 4 mjini Marrakech tayari kwa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Green Buffalos kutoka Zambia utakaopigwa kesho saa nne usiku.

Uwanja tuliofanyia mazoezi ni maalumu kwa ajili hiyo na upo nje ya dimba ambalo tutalitumia kwa mchezo huo muhimu ambao tunahitaji ushindi ili kufuzu hatua ya nusu fainali.

Wachezaji wote wamefanya mazoezi na wapo kwenye hali nzuri tayari kupambania ushindi na kuzidi kuweka historia kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Mchezo wa kesho ni kama fainali na wachezaji wetu wameandaliwa kimwili na kiakili kwa ajili ya kuhakikisha tunashinda ingawa haitakuwa mechi rahisi.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER