Simba Queens imefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Brimo Meda kujiandaa na mchezo wa kesho wa Nusu Fainali dhidi ya Polisi Bullets kutoka Kenya.
Mchezo huo wa Nusu Fainali ambao tunatarajia utakuwa mgumu utapigwa kesho saa tano asubuhi katika Uwanja wa Abebe Bikila.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo huo muhimu ambao lengo letu ni kushinda ili kutinga fainali.
Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anaipambania timu kufikia malengo yake.