Queens yafanya mazoezi ya mwisho

Kikosi cha Simba Queens kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Veterani kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi ya Alliance Girls.

Mchezo huo ambao utapigwa katika Uwanja wa Azam Complex saa 10 jioni.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna ambaye tutamkosa kutokana nakuwa majeruhi au kutumikia adhabu ya kadi.

Baada ya kucheza mechi mbili za ugenini dhidi ya Amani Queens na Bunda Queens kikosi chetu kimerejea katika Uwanja wa nyumbani kuwakabili Alliance Girls.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER