Queens yafanya mazoezi ya kwanza Morocco

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya kwanza tangu kiwasili nchini Morocco leo jioni katika Uwanja wa Academia Fus Rabat.

Baada ya timu kufika Morocco jana jioni wachezaji walipewa mapumziko kwa ajili ya uchovu wa safari na leo wameanza mazoezi rasmi.

Benchi la ufundi chini ya Kocha Charles Lukula limeridhishwa na jinsi wachezaji wanavyojituma mazoezini hivyo matumaini ya kufanya vizuri ni makubwa.

Mchezo wetu wa kwanza kwenye mashindano haya utakuwa Jumapili, Oktoba 30 dhidi ya wenyeji ASFAR FC.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER