Queens yafanya ‘mauaji’ Lindi

 

Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Amani Queens katika mchezo wa Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League uliopigwa Uwanja wa Nyangao Sekondari, Lindi.

Mshambuliaji Asha Djafar alitupatia bao la kwanza dakika ya sita baada ya kuwapiga chenga walinzi wa Amani na kupiga shuti ambalo lilimshinda mlinda mlango.

Nahodha Opa Clement alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya tisa baada ya mchezaji mmoja wa Amani kuunawa mpira ndani ya 18.

Opa tena alitupatia bao la tatu dakika ya 30 baada ya kupiga shuti ambalo lilizuiliwa na mlinda mlango kabla ya mpira kumkuta tena na kumalizia.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ile ile ambao Jentrix Shikangwa alifunga mabao mawili ya haraka dakika za 50 na 60.

Zaina Mohamed ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Opa Clement naye alifunga mabao mawili ya haraka ndani ya dakika moja 70, 71 na kukamilisha karamu ya mabao.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Asha Djafar, Pambani Kuzoya, Vivian Corazone, Opa, na Dotto Evarist na kuwaingiza Mwanahamisi Omary, Olaiya Barakat, Jackline Albert na Zaina Mohamed

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER