Kikosi cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Amani Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Mchezo ulikuwa mkali huku timu zikishambuliana kwa zamu lakini hakuna aliyeweza kutumia nafasi na kufanya kwenda mapumziko bila kufungana.
Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kuongeza mashambulizi na dakika ya 60 tulipata bao la kwanza kupitia kwa mlinzi Ruth Ingosi.
Jentrix Shikangwa alitupatia bao la pili dakika ya 78 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Asha Djafar.
Kocha Musa alifanya mabadiliko ya kuwatoa Elizabeth Wambui, Violeth Nicholas, Daniella Ngoyi, Dotto Evarist na kuwaingiza Fatuma Issa, Esther Mayala na Joanitah Ainembabazi.
Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 14 tukiendelea kubaki kileleni mwa msimamo.