Queens yaendelea kutoa dozi TWPL

Timu yetu ya Simba Queens imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bunda Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu ambapo Aisha Mnuka alitupatia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 42.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi ambapo tulipata mabao mawili haraka yote yakifungwa na Jentrix Shikangwa dakika za 58 na 62.

Asha Djafar alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne dakika ya 87 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Bunda.

Kocha Mussa Hassan Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Mwanahamisi Omary, Jentrix Shikangwa na Vivian Corazone na kuwaingiza Asha Djafar, Zainab Mohamed na Zubeda Mgunda.

Queens imefikisha pointi 43 baada ya kucheza mechi 15 ikiwa kileleni mwa msimamo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER