Queens yaanza kwa kishindo SWPL

Kikosi chetu cha Simba Queens kimeanza vema Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Ceasiaa katika mchezo uliopigwa Uwanja Azam Complex.

Queens ilianza mchezo kwa kasi na kuliandama lango la Ceasiaa ambao muda mwingi walikuwa wakizuia.

Katika ushindi huo mshambuliaji Aisha Juma amefunga mabao matatu ‘hat trick’ nakuwa mwiba mchungu kwa walinzi wa Ceasiaa.

Mabao mengine ya Queens yaliwekwa kambani na Asha Djafar na Mwanahamisi Omary aliyeingia kipindi cha pili.

Kocha Mkuu Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Violeth Nicholas, Asha Rashid, Ruth Ingosi na Vivian Corazone na kuwaingiza Koku Kipanga, Mwanahamisi Omary, Fatuma Issa, Joanitah Ainebambazi na Joelle Bukuru.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER