Queens mabingwa CECAFA

Timu yetu ya Simba Queens imetawazwa Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA baada ya kuifunga SHE Corporates kutoka Uganda bao moja katika mchezo wa fainali uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo ulikuwa mkali na wa kuvutia kutokana na timu zote kujuana vizuri kwani tulishakutana katika hatua ya makundi na tukaibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Pamoja na kupata ushindi huo lakini tulikuwa na uwezo wa mabao mengi zaidi kama tungeongeza umakini katika nafasi tulizotengeneza.

Mlinda mlango wa SHE Corporates ameonyesha kiwango bora kwa kuokoa michomo ya washambuliaji ambapo kama asingekuwa makini dhahama kubwa ingewakuta mabingwa hao wa Uganda.

Kiungo mkabaji Vivian Corazone alitupatia bao hilo pekee kwa mkwaju wa penati dakika ya 47 ambalo limetuhakikishia kubakisha taji katika ardhi ya nyumbani.

Ubingwa huu unatufanya kupata tiketi ya kuiwakilisha Ukanda wa CECAFA katika Ligi ya Mabingwa Afrika na tunakuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kufanya hivyo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER