Queens kuondoka kesho kuifuata Fountain Gate Dodoma

Kikosi cha wachezaji 24 wa Simba Queens kitaondoka kesho asubuhi kuelekea jijini Dodoma kuifuata Fountain Gate Princess kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL).

Mchezo huo utapigwa Ijumaa, Februari 2 katika Uwanja wa Jamhuri jijini humo ikiwa tunaenda kwa lengo moja la kutafuta alama tatu.

Queens imefanya mazoezi ya mwisho jijini Dar es Salaam jioni katika Uwanja wa Veterani kujiweka sawa kabla ya kesho kuanza safari.

Queens itaondoka kuelekea Dodoma ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi mnono wa mabao 7-0 tuliopata katika mchezo uliopita dhidi ya Alliance Girls siku tatu zilizopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER