Queens kuondoka Kesho Alfajiri kuifuata Mkwawa Iringa

Kikosi chetu cha Simba Queens kesho alfajiri kitasafiri kuelekea mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) dhidi ya Mkwawa Queens utakaopigwa Januari 11.

Mchezo huo ambao tunategemea utakuwa mgumu na wenye ushindani kutokana na ubora wa timu zote utapigwa katika Uwanja wa Samora saa 10 jioni.

Kocha mkuu, Charles Lukula amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri morali ya wachezaji ipo juu tayari kuhakikisha tunapambana kupata alama tatu.

Lukula amesema ushindi tuliopata dhidi ya Fountain Gate Jumanne iliyopita umeongeza ari kwa wachezaji ambayo anaamini itatufanya kupata ushindi.

“Tunaondoka kesho alfajiri kuelekea Iringa kwa mchezo wa Jumatano dhidi ya Mkwawa Queens, tunataraji utakuwa mchezo mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

“Ligi ya msimu huu ni ngumu, ushindani umeongezeka kila timu imejiandaa vizuri lakini sisi ni mabingwa watetezi hivyo tunahitaji kufanya vizuri kwenye kila mchezo,” amesema Lukula.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER