Queens kufungua pazia la SLWPL na JKT kesho

Timu yetu ya Simba Queens kesho itaanza kampeni ya kutetea taji la Ligi Kuu ya Wanawake Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) kwa kucheza na JKT Queens katika mchezo utakaopigwa Mo Simba Arena.

Queens ilianza maandalizi ya ligi hii inayoanza kesho Novemba 24 siku chache baada ya kurejea kutoka nchini Morocco ilipokuwa inashiriki Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa na wachezaji wapo kwenye hali nzuri wanasubiri kesho saa 10 jioni kutupa karata ya kwanza dhidi ya JKT.

Tunafahamu ligi itakuwa ngumu hasa kwetu ukizingatia sisi ni mabingwa mara tatu mfululizo kwa hiyo timu zitajipanga zaidi zikicheza nasi lakini tumejiandaa kikamilifu kuzikabili.

JKT ni timu nzuri imekaa pamoja muda mrefu na inatupa upinzani mkubwa kila tukikutana lakini tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunawakabili na kuanza kwa pointi tatu kesho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER