Queens kufungua pazia la Klabu Bingwa Afrika leo

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens leo itashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Garde Republicaine FC ya Djibouti katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Mchezo huo wa Kundi B utaanza saa moja usiku ambapo malengo yetu ni kuhakikisha tunachukua ubingwa huu katika ardhi ya nyumbani.

Jumatano kikosi cha Queens kitashuka katika Uwanja wa Azam Complex kuikabili SHE Corporates ya Uganda saa 10 jioni.

Mchezo wa mwisho katika hatua ya makundi utakuwa Jumapili dhidi ya Yei Joint Stars ya Sudan ya Kusini utakaopigiwa Azam Complex saa moja usiku.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER