Queens kuanza safari ya kurejea nyumbani

Baada ya kuwepo nchini Morocco takribani wiki tatu kushiriki Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kikosi chetu leo kimeanza safari ya kurejea nyumbani.

Saa nne asubuhi kikosi kitaondoka katika Mji wa Rabat kuelekea jijini Casablanca ambapo kitapanda ndege mpaka nchini Uturuki.

Kikosi kitafika Uturuki saa nne usiku na watalala nchini humo kabla ya kubadili ndege Jumanne usiku kisha kuanza safari rasmi ya kurejea nyumbani.

Kikosi kinatarajia kufika jijini Dar es Salaam saa nane usiku wa kuamkia Jumatano Novemba 16.

Queens imeshiriki michuano hiyo mikubwa Afrika kwa mara ya kwanza na imemaliza nafasi ya nne ikiwa ni timu ya kwanza kutoka Afrika Mashariki kufika hatua hiyo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER