Queens kamili kwa Derby Jumapili

Kikosi chetu cha Simba Queens kipo kwenye maandalizi makali kuelekea mchezo wa Derby dhidi ya Yanga Princess wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) utakaopigwa Jumapili saa 10 jioni.

Meneja wa timu Seleman Makanya amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo huo muhimu na hakuna mchezaji yoyote aliyepata majeraha.

Makanya amesema mchezo dhidi ya Yanga ni muhimu kushinda kwani ukiacha kupata alama tatu bali pia kuweka heshima hivyo amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kupata burudani.

Makanya ameongeza kuwa soka la wanawake linazidi kupanda chati siku hadi siku na ushindani umeongezeka hivyo amewasisitiza mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu.

“Maandalizi ya mchezo wetu wa Derby yanaendelea vizuri, wachezaji wapo kwenye hali nzuri hakuna majeruhi. Tunachohitaji ni mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kuja kutupa sapoti.

“Tumedhamiria kutetea ubingwa wetu lakini itakuwa vizuri kama tutawafunga watani Jumapili ndiyo maana nasisitiza mashabiki waje kwa wingi uwanjani,” amesema Makanya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER