Queens Kamili dhidi ya Wasudan CECAFA

Kikosi chetu cha Simba Queens kipo tayari kwa mchezo wa kesho wa kukamilisha hatua ya makundi ya klabu bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya Yei Joint Stars kutoka Sudan Kusini ili kutinga hatua hiyo kibabe.

Queens imeshinda mechi zote mbili za kwanza dhidi ya Garde Publicaine ya Djibouti na SHE Corporates ya Uganda tukifunga mabao nane huku tukiwa hatujaruhusu hata moja.

Kocha Mkuu Sebastian Nkoma, amesema kikosi kipo tayari na wachezaji wapo kwenye hali nzuri huku wakimuhakikishia kupambana na kupata ushindi.

Nkoma amesema malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda michuano hii ili kuitangaza vema nchi kwakuwa michuano inafanyika katika ardhi ya nyumbani.

“Wachezaji wapo kwenye hali nzuri, tutakosa huduma ya mchezaji mmoja ambaye ni majeruhi. Lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kesho ili kuingia nusu fainali tukiwa hatujapoteza mchezo wowote na hii itatuongezea morali kuelekea hatua inayofuata,” amesema Nkoma.

Mchezo huo wa kundi B utapigwa saa 9 alasiri katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER