Queens ipo tayari kwa Ligi ya Mabingwa Afrika

Kocha Mkuu Charles Lukula amesema kikosi chetu kipo tayari kwa mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji ASFAR FC ya Morocco utakaopigwa kesho saa nne usiku kwa saa za nyumbani.

Lukula amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kupigania bendera ya nchi.

Kocha Lukula ameongeza kuwa ingawa ndiyo mara yetu ya kwanza kushiriki michuano hii mikubwa Afrika lakini kikosi kipo tayari kutoa ushindani.

“Tupo tayari kwa michuano hii mikubwa, kabla ya kuja tulikuwa tunajua tutakutana na timu nzuri nasi tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri,” amesema Lukula.

Kwa upande wake kiungo mkabaji Vivian Corazone amesema morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja amejitahidi kufanya vizuri mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa mashindano tunajua itakuwa migumu lakini tuna uzoefu na tupo tayari kwa mapambano,” amesema Corazone.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER