Timu yetu ya Simba Queens imebakisha alama moja tu kabla ya kutawazwa Mabingwa na kurejesha taji la Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) ambalo tulilipoteza msimu uliopita.
Queens ipo killeni mwa msimamo ikiwa na pointi 43 alama tisa juu ya JKT Queens ambayo ipo nafasi ya pili.
Mpaka sasa kila timu imecheza mechi 15 na kusalia na michezo mitatu pekee.
Hizi hapa mechi zetu tatu zilizosalia:
Juni 7
Alliance Girls Vs Simba Queens
Uwanya wa Nyamagana saa 10 Jioni
Juni 10
Simba Queens Vs Fountain Gate Princess
Uwanja wa Azam Complex saa 10 Jioni
Juni 14
Simba Queens Vs Geita Queens
Uwanja wa Azam Complex saa 10 Jioni