Queens iko tayari kwa Nusu Fainali CECAFA Kesho

Nahodha wa timu yetu ya Simba Queens, Fatuma Issa ‘Fetty Densa’ amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) dhidi ya AS Kigali ya Rwanda kesho.

Fetty Densa amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani hao lakini tuko tayari kuhakikisha tunashinda na kutinga fainali.

Fetty ameongeza kuwa msimu uliopita tuliishia hatua hii katika michuano iliyofanyika nchini Kenya lakini kwa sasa tuko ardhi ya nyumbani mbele ya mashabiki wetu tunaamini tutashinda na kutinga fainali.

“Sisi tuko tayari, wachezaji wote tupo kwenye hali nzuri, morali ipo juu na lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kesho na kutinga fainali.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tupo nyumbani mbele ya viongozi wetu na mashabiki kwa hiyo hatutaki kuwaangusha,” amesema Fetty Densa.

Mchezo huo ambao utakuwa ni nusu fainali ya pili utapigwa katika uwanja wa Azam Complex saa moja usiku.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER