Queens haishikiki yaichakaza Ilala ‘5G’

Timu yetu ya Simba Queens imeendeleza umwamba katika Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Womens Premier League) baada ya kuifunga Ilala Queens mabao 5-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Mo Simba Arena.

Tulianza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata mabao ya haraka dakika ya pili na 15 kupitia kwa mshambuliaji kinara Asha Djafar.

Mercy Tagoe aliyeingia kutokea benchi alitupatia bao la tati dakika ya 75 kabla ya kiungo fundi Joelle Bukuru akitupa la nne dakika tano baadae.

Mercy alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la tano dakika ya 90 na kutuhakikisha alama tatu muhimu katika uwanja wa nyumbani.

Kocha wa Queens, Sebastian Nkoma alimtoa Jacline Albert Violeth Thadeo na kumuingizaa Mecy Tagoe na Julieta Singano

Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 42 baada ya kushinda mechi zote 14 za ligi tulizocheza.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER