Queen yapoteza kwa Yanga Princess

Timu yetu ya Simba Queens imepoteza kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kulala kwa bao moja mbele ya Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu lakini umakini wa kumalizia nafasi zilizopatikana ikawa changamoto.

Mlinzi wa kati Juliet Singano alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya nne baada ya kumchezea faulo Clara Luvanga.

Clara aliwapatia bao hilo Yanga Princess dakika ya 45 baada ya kupiga shuti ambalo lilimgonga mlinda mlango wetu Gelwa Yona kabla ya kuingia wavuni.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi kutafuta bao la kusawazisha lakini bahati haikuwa upande wetu kutokana na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga.

Kocha Sebastian Nkoma aliwatoa Jackline Albert, Wema Richard na Asha Djafar na kuwaingiza Amina Ramadhani, Koku Kipanga na Mercy Tagoe.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER