Preview: Mchezo wetu dhidi ya Vipers

Leo saa moja usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa St. Mary’s jijini Entebe, Uganda kuikabili Vipers katika mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Kivutio kikubwa katika mchezo wa leo ni uwepo wa kocha wetu mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ambaye aliiwezesha Vipers kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kujiunga nasi.

Robertinho anaujua vizuri Uwanja wa St. Mary’s wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 15,000 pamoja na Vipers kwa ujumla kwakuwa amedumu hapo kwa takribani mwaka mzima.

Katika Mkutano wa Waandishi wa Habari kabla ya mchezo Robertinho alinukuliwa akisema itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunaondoka na pointi zote tatu.

Ushindani mwingine utatokana na nafasi ya timu zote zilipo kwakuwa hakuna iliyowahi kupata pointi tatu.

Ni mechi ya kufa au kupona kwetu…

Katika mchezo wa leo tunahitaji kupata alama tatu ili kurejesha matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali. Tumetoka kupoteza mechi mbili ikiwemo moja nyumbani hivyo matokeo ya ushindi ndio kitu tunahitaji.

Hali ya Kikosi..

Wachezaji wapo kwenye hali nzuri, morali ipo juu na wanafahamu ugumu na umuhimu wa mchezo wa leo na wapo tayari kupambana hadi jasho la mwisho kuwapa Wanasimba furaha.

Wachezaji wote 24 tuliokuja nao wameshiriki mazoezi ya mwisho jana jioni na wapo kwenye hali nzuri na hakuna yoyote ambaye amepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo.

Kanoute arejea.

Kiungo Mkabaji, Sadio Kanoute aratakuwa sehemu ya mchezo wa leo baada ya kukosa mechi iliyopita dhidi ya Raja Casablanca kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER