Preview: Mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting

Leo saa moja usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi kuu ya NBC.

Ingawa Ruvu haipo kwenye nafasi nzuri katika msimamo hilo halitupi kiburi badala yake tutaingia kwa kuwaheshimu kwakuwa lengo letu ni moja kuhakikisha tunashinda.

Wakati ligi ikiwa inaelekea ukingoni kila timu inapigania kupata alama tatu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi nasi malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zote zilizobaki.

Mapema jana Kocha Mkuu Roberto Oliveira ‘Robertinho’ aliweka wazi mbele ya Waandishi wa Habari kuwa bila kujalisha tutapata nini msimu huu tunapaswa kushinda kila mchezo uliosalia.

“Simba ni timu kubwa, ina wachezaji weredi haitakuwa vizuri kumaliza mechi za ligi zilizobaki bila kupata ushindi.

“Tuna wachezaji wakubwa ambao hawaitaji kuambiwa wanatakiwa kufanya nini kwenye mechi, jana nilikaa nao tukaongea kuhusu hili. Nawaamini wachezaji wangu,” amesema Robertinho.

Hali ya kikosi.

Wachezaji wapo kwenye hali nzuri, jana wamefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena tayari kwa mchezo wa leo.

Wachezaji wote ambao walikuwa sehemu ya mchezo uliopita wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup wameshiriki mazoezi ya jana na wapo tayari.

Manula bado hayupo fiti.

Mlinda mlango namba moja, Aishi Manula ataendelea kukosekana katika mchezo wa leo kutokana na kuendelea kuuguza jeraha alilopata mwezi uliopita.

Tuliwafunga 4-0 kwa Mkapa.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Novemba 19 tuliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Katika mchezo huo nahodha John Bocco alifunga mabao matatu ‘hat trick’ huku moja likifungwa na mlinzi, Shomari Kapombe.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER