Preview: Mchezo wetu dhidi ya Namungo

Leo saa moja usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa Lindi kuikabili Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tunaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mechi yetu ya mwisho ya ligi dhidi ya Ihefu FC iliyofanyika katika  Uwanja wa Highland Estate.

Wachezaji wote wamesafiri kuja Lindi wameshiriki mazoezi ya mwisho yaliyofanyika jana usiku katika Uwanja wa Majaliwa.

Kocha Msaidizi Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.

Mgunda amesema tunafahamu mchezo utakuwa mgumu na tunaiheshimu Namungo hasa tukijua wapo nyumbani lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu, tunawaheshimu Namungo ni timu nzuri ina wachezaji bora na wapo nyumbani haitakuwa rahisi lakini tuko tayari,” amesema Mgunda.

Tuliwafunga Mzunguko wa kwanza.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Novemba 16, 2022 tuliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kwa sasa lengo letu ni kuhakikisha tunapambana kushinda mechi zetu zote zilizosalia za ligi ili kuzidi kujiweka kwenye mazingira mazuri.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER