Preview: Mchezo wetu dhidi ya Mtibwa

Leo Saa 10 jioni kikosi chetu kitacheza na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Uwanja wa Manungu Complex.

Kikosi chetu kitashuka kikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mechi tatu mfululizo mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers na Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya African Sports.

Tunaenda kukutana na Mtibwa ikiwa na uhitaji mkubwa wa pointi tatu kutokana na nafasi iliyopo lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunaondoka na pointi tatu.

Kocha msaidizi, Juma Mgunda amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri na wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo.

Mgunda ameenda mbali zaidi na kusema tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mtibwa lakini tumejipanga kila kitu.

“Ligi inaelekea ukingoni na kila timu inajipanga kuhakikisha inapata pointi tatu, tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mtibwa lakini tumejipanga kupambana kupata pointi tatu,” amesema Mgunda.

Tuliwafunga 5-0 Kwa Mkapa.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 30 tuliwafunga mabao 5-0.

Mabao yetu yalifungwa na Mzamiru Yassin, Augustine Okrah, Pape Sakho aliyefunga mawili na Moses Phiri.

Kadi nyekundu zilikuwa mbili.

Katika mechi hiyo wachezaji wawili wa Mtibwa walitolewa kwa kadi nyekundu kutokana na mchezo usio wa kiungwana.

Wachezaji hao ni Pascal Kitenge aliyetolewa dakika ya 42 na Cassian Ponela aliyetolewa dakika ya 72.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER