Preview: Mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ leo atakiongoza kikosi chetu kwa mara ya pili kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri saa moja usiku.

Mchezo wa leo utakuwa wa kwanza wa ugenini kwa Robertinho kwa kuwa ule wa kwanza dhidi ya Mbeya City iliyomalizika kwa ushindi wa mabao 3-2, Januari 18 tulikuwa nyumbani Benjamin Mkapa.

Katika mchezo wa leo pia benchi la ufundi limeongezewa nguvu baada ya kutua Kocha Msaidizi Ouanane Sellami raia wa Tunisia ambaye anaungana na Robertinho na Juma Mgunda.

Hali ya Kikosi

Tumesafiri na wachezaji 19 ambao wote wamefanya mazoezi na mwisho jana tayari kwa mchezo wa leo na hakuna yeyote ambaye amepata maumivu yatakayomfanya kukosa mchezo.

Tutawakosa nyota tisa katika mchezo wa leo kutokana na majeruhi huku wengine wakiwa wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Wachezaji wanaotumikia adhabu ya kadi tatu za njano: Sadio Kanoute, Joash Onyango, Pape Sakho na Mzamiru Yassin.

Wachezaji majeruhi: Moses Phiri, Peter Banda, Henock Inonga, Clatous Chama na Jonas Mkude.

Nyota wapya kuanza kuonekana leo

Wachezaji watatu ambao tumewasajili mwishoni mwa dirisha dogo la usajili Ismael Sawadogo, Jean Baleke na Mohamed Mussa watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani leo.

Nyota hao ni miongoni mwa wachezaji 19 waliopo Dodoma na benchi la ufundi litaamua kama wataanza moja kwa moja au watatokea benchi kulingana na utimamu wao wa mwili kwakuwa wamefanya mazoezi ya pamoja na wenzao kwa siku mbili tu.

Tuliwafunga 3-0 kwa Mkapa

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 2, tuliibuka na ushindi mabao 3-0.

Mabao yetu yalifungwa na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ aliyejifunga, Moses Phiri na Habib Kyombo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER