Preview: Mchezo wetu dhidi ya Coastal Union

Leo 9:30 Alasiri kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Uhuru kuikabili Coastal Union katika mchezo wa Ligi ya NBC ambao utakuwa wa mwisho katika msimu wa 2022/23.

Maandalizi ya mchezo yamekamilika kwa asilimia kubwa na wachezaji wapo kwenye hali tayari kuipigania timu kupata pointi zote tatu.

Ingawa matokeo mchezo hayataathiri chochote kwetu kutokana na alama tulizokusanya mpaka sasa lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Kauli ya Kocha msaidizi Juma Mgunda…..

“Maandalizi kwa ajili ya mchezo yamekamilika, wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa kuipambania timu kupata alama tatu.

“Tunajua itakuwa mechi ngumu, Coastal ni timu nzuri na inahitaji ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri nasi malengo yetu ni kushinda kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Mgunda.

Hali ya Kikosi….

Katika mchezo wa leo tutaendelea kuwakosa viungo wetu Clatous Chama na Sadio Kanoute ambao wanatumikia adhabu ya kufungiwa kikakuni.

Kiungo mshambuliaji Pape Sakho nae hatakuwa sehemu ya mchezo kutokana na kuwa tayari amejiunga na timu yake ya Taifa ya Senegal inayojiandaa na mechi za kufuzu michuano ya AFCON.

Tuliwafunga 3-0 Mzunguko wa kwanza….

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa CCM Mkwakwani uliopigwa Desemba 3 tuliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Mabao yetu yalifungwa na Moses Phiri aliyefunga mawili na Clatous Chama.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER