Preview: Horoya vs Simba CAFCL

Baada ya kupita takribani miezi minne kasoro wiki moja tangu tulivyocheza mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika leo tunacheza ugenini dhidi ya Horoya ya Guinea.

Hii ni mara yetu ya kwanza kukutana na Horoya katika historia yetu, hatujawahi kucheza nao kabla wala hatujawahi kucheza mechi yoyote ya kimashindano nchini Guinea.

Mchezo wa leo utakuwa wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kocha mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ kukiongoza kikosi sababu mechi zote nne za hatua ya awali timu ilikuwa chini ya kocha Juma Mgunda.

Mchezo wa leo pia utakuwa ni wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wachezaji Jean Baleke, Ismael Sawadogo na Mohamed Mussa ambao tumewasajili katika dirisha dogo.

Safari yetu ya Ligi ya Mabingwa ilianza hivi….

Mara ya mwisho kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa Oktoba 16 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa tulipoibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Primeiro de Agosto ya Angola.

Katika mechi zote nne za hatua ya awali tulizocheza tumeibuka na ushindi tukifunga mabao nane na kuruhusu bao moja pekee.

Matokeo ya mechi za hatua ya awali…….

Septemba 10, Nyasa Big Bullets 0-2 Simba

(Moses Phiri, John Bocco)

Septemba 18, Simba 2-0 Nyasa Big Bullets

(Moses Phiri yote)

Oktoba 9, Primeiro de Agosto 1-3 Simba

(Clatous Chama, Israel Patrick, Moses Phiri)

Oktoba 16, Simba 1-0 Primeiro de Agosto

(Moses Phiri)

Jenerali Moses Phiri ndiye kinara.

Katika mechi nne za hatua ya awali mshambuliaji Moses Phiri amefunga katika michezo yote huku akitupia kambani mabao matano.

Nahodha John Bocco, Clatous Chama na mlinzi Israel Patrick wamefunga bao moja kila mmoja.

 

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER