Pointi moja tu tuchukue ubingwa wa VPL leo

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku kuikabili Coastal Union kwenye mchezo wa ligi kuu ambao tukipata hata sare tutatangazwa mabingwa kwa mara ya nne mfululizo.

Alama moja kwenye mchezo wa leo itatufanya kufikisha pointi 77 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

Kimahesabu tungeweza kutangzawa mabingwa baada ya mchezo dhidi ya KMC juzi lakini sababu wanaotufuata wanaweza kuzifikia pointi 66 tulizonazo ingawa tumewaacha mbali kwenye uwiano wa mabao ya kufunga ndiyo maana tunahitaji alama moja leo kuwa mabingwa.

Licha ya hivyo, tutaingia uwanjani kwa lengo la kusaka pointi tatu ili kuonyesha tumestahili kuwa machampioni.

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema anaamini mchezo utakuwa mgumu kwa sababu Coastal wanahitaji alama tatu ili kujinusuru na janga la kushuka daraja wakati sisi tunahitaji moja tu tutangazwe mabingwa.

“Sisi tunahitaji alama moja ili tutangazwe mabingwa na wao wanahitaji pointi tatu kujinusuru, kwa hiyo haiwezi kuwa mechi rahisi. Ukiachana na matokeo yao bado Coastal inacheza soka safi na tunatarajia kupata ushindani mkubwa,” amesema Matola.

TAARIFA YA KIKOSI

Katika mchezo wa leo tutakosa huduma za mlinzi Joash Onyango ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano na Bernard Morrison aliyepewa ruhusa kwenda nchini kwao Ghana.

Wachezaji wengine wote wapo tayari na kamili kwa ajili ya kuweka historia ya kuchukua ubingwa kwa mara nne mfululizo.

MCHEZO ULIOPITA TULIVYO KUTANA

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha tuliibuka na ushindi wa mabao 7-0. Mabao hayo yalifungwa na John Bocco aliyefunga ‘hat trick’ Clatous Chama amefunga mawili, Hassan Dilunga na Bernard Morrison.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER