Phiri nje wiki moja

Majibu ya vipimo vya MRI na X ray aliyofanyiwa mshambuliaji wetu kinara Moses Phiri yamekamilika na imeonekana ameumia.

Kwa majibu hayo Phiri atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki moja hadi mbili kuuguza jeraha hilo ambalo si kubwa lakini anapaswa kuwa chini ya uangalizi ili kupona kabisa.

Phiri atakosa mechi zetu mbili za kufungia mwaka 2022 dhidi ya KMC itakayopigwa Jumatatu ijayo na ule wa Disemba 30 dhidi ya Tanzania Prisons.

Phiri ni miongoni mwa wachezaji wetu wawili walioocheza mechi zote 15 za mzunguko wa kwanza wa ligi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER