Phiri: Najisikia furaha kuwa sehemu ya mafanikio haya madogo

Mshambualiaji wetu mpya Moses Phiri, amefunguka kuwa anafurahia kuwa sehemu ya mafanikio tuliyopata katika mechi mbili za kwanza za ligi.

Phiri amesema anafurahia kuwa sehemu ya mabao matano tuliyofunga na kutufanya tuwe kileleni mwa msimamo ambapo mpaka sasa yeye ametupia mawili.

Nyota huyo raia wa Zambia amesema sapoti tunayopata kutoka kwa mashabiki wetu inaongeza morali na kuwafanya kujituma uwanjani kupigania alama tatu.

Phiri ameongeza lengo lake ni kuhakikisha anatumia kila nafasi atakayopata uwanjani kufunga ili kuwapa furaha mashabiki ambao mara zote wapo upande wetu.

“Nina furaha kuwa sehemu ya familia hii ya Simba, nina furaha pia kuwa sehemu ndogo ya mafanikio tuliyopata mpaka sasa yanayotufanya tuwe kileleni mwa msimamo wa ligi.

“Mashabiki mmekuwa na msaada mkubwa kwetu, sapoti yenu kwetu inatuongezea morali wa kuendelea kupambana ili kuwapa furaha,” amesema Phiri.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER