Phiri Mchezaji Bora wa Mashabiki Septemba

Mshambuliaji Moses Phiri amefanikiwa kushinda kinyang’anyiro cha Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Septemba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Phiri ameshinda kinyang’anyiro hicho baada ya kuwashinda nyota wawili ambao ni viungo Clatous Chama na Mzamiru Yassin ambao aliingia nao fainali.

Katika mwezi Septemba Phiri amecheza mechi nne akifunga mabao matatu na kusaidia mengine mawili baada ya kucheza dakika 334.

Mchanganuo wa kura zilivyopigwa

Kura Asilimia

Phiri     3564     73.97
Chama 1089      22.60
Mzamiru 165      3.42

Kwa kushinda tuzo hiyo Phiri atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

Phiri anakuwa mchezaji wa pili kushinda tuzo hiyo msimu huu katika kikosi chetu baada ya Chama kufanya hivyo mwezi Agosti.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER