Phiri: Kusafiri na Mashabiki kwenda Ndola kunatupa hamasa wachezaji

Mshambuliaji, Moses Phiri amesema kitendo cha mashabiki kusafiri kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Ndola, Zambia itawapa wachezaji hamasa kuelekea mchezo wa Jumamosi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos.

Phiri amesema mashabiki wana nafasi kubwa ya kuifanya timu kufanya vizuri kwakuwa mara zote wachezaji wanajiona wana deni kwao.

“Tunafurahi kuona tunasafiri na mashabiki kutoka Dar es Salaam, hii itakuwa chachu kubwa kwetu kuhakikisha tunapambana kuwapa furaha mashabiki ambao wametoka nyumbani kuja kutupa sapoti sisi,” amesema Phiri.

Akizungumzia mchezo wenyewe Phiri amesema “itakuwa mechi ngumu, Dynamos ni timu bora na ipo nyumbani ukizingatia siku chache zilizopita tumecheza nao kwahiyo tunafahamiana vizuri.”

Phiri ambaye tumemsajili kutoka Zanaco ameongeza kuwa kuna kumbukumbu nyingi kila mara anaporudi kucheza nyumbani kwao Zambia hasa anapokutana na Power Dynamos.

“Kumbukumbu zipo nimewahi kucheza dhidi ya Power Dynamos, nafurahi kucheza kwenye ardhi ya nyumbani lakini nipo tayari kuipigania timu yangu ya Simba kupata ushindi,” amemalizia Phiri.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER