Phiri kama kawa atupia mawili tukiitoa Big Bullets

Mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Moses Phiri yametosha kutuvusha na kutinga hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga Nyasa Big Bullets 2-0 mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Tulianza mchezo kwa kasi na kuliandama lango la Bullets tukiwa na lengo la kutafuta bao la mapema lakini tulikosa umakini katika kumalizia nafasi.

Moses Phiri alitupatia bao la kwanza dakika ya 29 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa ‘fundi’ Clatous Chama.

Phiri tena alitupatia bao la pili dakika ya 50 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Augustine Okrah kufuatia shambulizi la kushtukiza lilipoanzia nyuma.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa Kibu Denis, Okrah, Phiri, Chama na Henock Inonga na kuwaingiza Pape Sakho, Peter Banda, Nelson Okwa, Mohamed Ouattara na Dejan Georgijevic.

Matokeo haya yanatufanya kufuzu hatua ya kwanza kwa jumla ya mabao 4-0 baada ya ushindi wa 2-0 tuliopata kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Malawi Jumamosi iliyopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER