Phiri awataja wachezaji wenzake Tuzo ya Septemba

Mshambualiaji wetu kinara Moses Phiri amewashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliompa hadi kufanikiwa kuibuka mshindi katika Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Septemba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Phiri amesema ushirikiano aliopata ni mkubwa kutoka kwa wenzake na anaamini ataendelea kufunga na kuchukua tuzo hiyo mara kwa mara kutokana na kuzungukwa na wachezaji bora.

Phiri ameibuka mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kuwazidi nyota wenzake wawili Clatous Chama na Mzamiru Yassin aliokuwa ameingia nao fainali.

“Nawashukuru wachezaji wenzagu kwa kunipokea na kunipa ushirikano ndani na nje ya pia nawashukuru mashabiki kwa sapoti yao na kunipigia kura zilizoniwezesha kupata tuzo hii.Tuzo hii inatuhamasisha sisi wachezaji kufanya vizuri na kuipigania timu.

“Naamini nikiendelea kupata sapoti kutoka kwa wachezaji wenzangu naweza kuchukua tuzo hii hata kila mwezi,” amesema Phiri.

Katika mwezi Septemba Phiri amecheza mechi nne akifunga mabao matatu na kusaidia mengine mawili baada ya kucheza dakika 334.

Kwa kushinda tuzo hiyo Phiri amekabidhiwa pesa taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER