Phiri atupia manne tukiichakaza Eagle kwa Mkapa

Mshambuaji kinara Moses Phiri amefunga mabao manne katika ushindi wa mabao 8-0 tuliopata dhidi ya Eagle FC kwenye mchezo wa hatua ya pili ya Azam Sports Federation Cup uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Habib Kyombo alitupatia bao la kwanza dakika ya tisa baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Clatous Chama na kumpiga chenga mlinzi wa Eagle kabla ya kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango.

Moses Phiri alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 14 baada ya Sadik Mack kuunawa mpira ndani ya 18 katika jitihada za kuokoa.

Phiri aliongea la tatu dakika ya 18 baada ya kupokea pasi mpenyezo kutoka kwa Mohamed Hussein na kuwazidi kasi walinzi wa Eagle na kuachia shuti lililomshinda mlinda mlango wa Eagle.

Phiri alikamilisha hat trick kwa kufunga bao la nne dakika ya 24 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Pape Sakho.

Dakika ya 28 Sakho alitupatia bao tano akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe kabla ya Chama kuongeza la sita dakika mbili baadaye.

Phiri aliongea la saba dakika ya 60 akipokea pasi safi ya Zimbwe Jr huku Chama akipiga la nane dakika ya 73 na kukamilisha karamu ya mabao.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa Kapombe, Mzamiru Yassin, Sakho, Phiri na Kyombo kuwaingiza Erasto Nyoni, Nelson Okwa na Augustine Okrah, Kibu Denis na Nassor Kapama.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER