Mshambuliaji kinara, Moses Phiri ameahidi kurejesha makali yake na kuendelea kufunga mabao baada ya kupona majeraha.
Phiri amesema ushindani wa namba umekuwa mkubwa baada ya kuongezwa wachezaji wapya lakini nitapambana kurudisha nafasi yangu.
“Nina furaha nimerudi, sio kitu kizuri kwa mchezaji kukosa mechi nyingi kutokana na majeruhi lakini nimejipanga kuhakikisha narudi kwa nguvu kama nilivyoanza msimu.
“Kwa sasa niko fiti baada ya mchezo dhidi ya Singida nitakuwa tayari kucheza, nimejipanga kuhakikisha naendeleza ubora wangu.
Akizungumzia kuhusu ujio wa mshambuliaji, Jean Baleke, Phiri amesema “ni mchezaji mzuri, ana kasi pia anajua kufunga naamini ataisaidia timu.”