Pablo: Tutatumia uzoefu kuwakabili KMC

Kocha Mkuu, Pablo Franco ameweka wazi kuwa kikosi chetu hakiko tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi saa 10 jioni.

Pablo amesema katika muda wa siku saba idadi kubwa ya wachezaji wetu waliugua hivyo hatukupata nafasi ya kufanya maandalizi kuelekea mchezo wa kesho hivyo tutatumia uzoefu kuwakabili KMC.

Raia huyo wa Hispania amesema baada ya kuwasili Tabora jana kikosi kilifanya mazoezi ya kuweka miili sawa na leo ndiyo tutafanya mazoezi kamili kuelekea mechi yenyewe hivyo hatukujiandaa vizuri.

Kutokana na changamoto hiyo Pablo amesema tumewaandaa wachezaji kimwili na kiakili kwa ajili ya mchezo huo ambao tunataraji utakuwa mgumu lakini tutahakikisha tunapambana kupata alama tatu.

“Hatukupata muda mrefu wa kujiandaa kutokana na changamoto ya ugonjwa iliyowapata wachezaji wetu, jana ndio tulifanya mazoezi ya kuweka miili sawa baada ya kufika Tabora ila leo tutafanya mazoezi ya mwisho jioni.

“Ni vile tu hatuna mamlaka ya kusema tuisogeze mbele hii mechi ndiyo maana tupo hapa leo na sisi ni weledi tutacheza pamoja kuwa tunafahamu mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa KMC lakini tutapambana kuhakikisha tupata alama tatu,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER