Pablo: Tunataka kuwapa furaha mashabiki kesho

Kocha Mkuu Pablo Franco amesema tumejiandaa vizuri kuelekea katika mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie na tupo tayari kuwapa furaha mashabiki wetu.

Pablo amesema tumepata muda mzuri wa kufanya mazoezi hivyo utimamu kwa wachezaji ni mkubwa tayari kupambana kuhakikisha tunashinda na kuingia robo fainali.

Pablo amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kesho licha ya changamoto ya muda ya kuanza mechi ili kusapoti timu huku akiwaahidi furaha.

“Jambo zuri ni kuwa tulipata muda mrefu wa kufanya maandalizi, wachezaji wote ukiacha Hassan Dilunga ambaye ni majeruhi na Clatous Chama ambaye haruhusiwi kucheza kutokana na kanuni ila wengine wako tayari kwa kwa mchezo.

“Kundi letu bado lipo wazi na kila timu ina nafasi ya kutinga robo fainali hivyo tutacheza kwa tahadhari na kutumia vizuri nafasi tutakazopata,” amesema Pablo.

Kwa upande wake nahodha msaidizi,l Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema mapungufu tuliyofanya katika mchezo wa kwanza yamefanyiwa kazi na kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mechi.

“Hata tukiwa kambini tunakumbushana umuhimu wa mchezo, tunaichukulia kama mechi muhimu ya msimu ya msimu, tunaamini tutashinda kikubwa mashabiki tunawaomba mjitokeze kwa wingi,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER