Pablo: Tunaenda kukutana na timu bora

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu kutokana na ubora wa ‘Wanalambalamba’ hao.

Pablo amesema maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mapambano na tunaamini utakuwa mgumu.

Ingawa Azam itawakosa baadhi ya wachezaji wake ambao wataenda kushiriki michuano ya AFCON, Pablo amesema anaamini wapo wengine ambao wataziba nafasi zao na hakuna mapungufu yatakayoonekana.

“Mchezo utakuwa mgumu, Azam ni timu nzuri na ina wachezaji bora lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo na kufungua mwaka vizuri,” amesema kocha Pablo.

Pablo ameongeza kuwa ingawa tuna historia nzuri tunapokutana na Azam lakini hiyo haitupi uhakika wa asilimia 100 kuibuka na ushindi kwa kuwa kila mchezo ni tofauti.

“Mchezo wa kesho utakuwa ni mwingine, una mbinu zake na jinsi ya kuuendea. Tumefanya vizuri zaidi yao huko nyuma lakini haitupi uhakika wa kushinda hivyo tumejipanga kuwakabili katika wakati uliopo,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER