Kocha Mkuu Pablo Franco, amefunguka kuwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Biashara United utakaopigiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani.
Pablo amesema Biashara ina kikosi bora na wachezaji wazuri mmoja mmoja hivyo tumejipanga kuhakikisha tunawadhibiti ili kupata ushindi.
Raia huyo wa Hispania ameongeza kuwa katika mchezo wa kesho tumejipanga kuonyesha kiwango safi uwanjani kupata ushindi na kuwafurahisha mashabiki wetu.
Pablo amesema nyota Rally Bwalya na Mzamiru Yassin ambao walikosekana katika mechi zetu za Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na masuala ya kifamilia wamerejea kikosini na wapo tayari kwa kesho.
“Mchezo utakuwa mgumu, Biashara ni timu nzuri, ina wachezaji wazuri mmoja mmoja. Tunahitaji kushinda ili kupunguza idadi ya pointi iliyopo dhidi ya wanaoongoza. Tunacheza katika Uwanja wa nyumbani na tunategemea kupata ushindi,” amesema Pablo.
One Response