Pablo: Tumewasisitiza wachezaji kutumia nafasi

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema amewasisitiza wachezaji kuhakikisha tunatumia vizuri nafasi tutakazopata ili kupata ushindi kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji.

Pablo amesema benchi la ufundi linaendelea kuhakikisha tunatumia vema nafasi tunazopata ili kupunguza presha na kucheza soka letu la kawaida la kuburudisha mashabiki.

Raia huyo wa Hispania ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu Dodoma ni timu nzuri inacheza kitimu na tumejipanga kupata upinzani mkubwa lakini tunahitaji kupata alama tatu.

“Tumewasisitiza wachezaji kuhakikisha tunatumia kila nafasi tutakayopata. Tunahitaji kufanya hivyo ili kujipunguzia presha na kucheza mpira wetu tuliowazoea.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu tumejipanga kucheza vizuri na kushinda, tutawatumia wachezaji ambao watakuwa tayari kimwili na kiakili tayari kwa mchezo,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER