Pablo: Tumepata mazoezi mazuri kabla ya kucheza na Mtibwa

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema timu imepata mazoezi mazuri kabla ya mchezo wetu wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar tofauti na ilivyokuwa kwenye mechi iliyopita.

Pablo ameyasema hayo muda mfupi kabla ya kikosi kuanza safari ya kuelekea mkoani Morogoro tayari kwa mtanange huo.

“Baada ya timu kutoka jijini Mbeya wachezaji wamepata siku mbili za kufanya mazoezi na kesho tutafanya ya mwisho kabla ya mchezo wa Jumamosi.

“Nafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini benchi la ufundi pamoja na wachezaji liko tayari kuhakikisha kila mmoja anatimiza majukumu yake ili ushindi upatikane.

“Jambo zuri ni kwamba tumepata muda wa kufanya mazoezi. Katika mechi iliyopita jambo hilo halikupatikana. Kesho pia tutapata muda wa kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo Jumamosi,” amesema.

Aidha, Pablo amekiri mchezo kuwa mgumu kutokana na kusafiri mfululizo kutoka Zanzibar, Mbeya kisha Morogoro lakini tumejipanga na tupo tayari kupambana kuhakikisha tunashinda.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER