Pablo: Tumekuja kuvunja mwiko wa ASEC

Ingawa wapinzani wetu ASEC Mimosas hawajawahi kupoteza mchezo nyumbani, Kocha mkuu Pablo Franco ameweka wazi kuwa tumejipanga kuvunja mwiko huo kesho.

Pablo amekiri ASEC ni timu nzuri na wanaweza kufanya chochote hasa wakiwa nyumbani lakini tumekuja kuhakikisha tunabadili historia hiyo.

Pablo ameongeza kuwa matokeo ya ushindi katika mchezo wa kesho yatatuhakikishia kuingia robo fainali ya michuano hii na ndiyo lengo letu la kwanza.

“ASEC ni timu nzuri wametuonesha walivyokuja Dar es Salaam lakini pia katika kundi letu wao wana uwezo wa kufanya chochote lakini tumejipanga kuhakikisha tunawadhibiti.

“Tumekuja kupambana kubadili historia yao ya kutofungwa nyumbani tunataka kuwa wa kwanza kuwafunga ASEC kwao,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER