Pablo: Tumefanya makosa yaliyotugharimu

Kocha Mkuu Pablo Franco, ameweka wazi kuwa tumefanya makosa ya kiulinzi yaliyoifanya Namungo kupata mabao mepesi katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 katika Uwanja wa Ilulu.

Pablo amesema sisi kama timu kubwa inayopambania ubingwa hatutakiwi kufanya makosa kama yale ambayo yanazidi kutuweka katika mazingira magumu.

Mbali na safu ya ulinzi kufanya makosa Pablo amesema pia hatukuwa vizuri katika kumalizia nafasi tulizopata hasa kipindi cha kwanza.

“Kwa timu kubwa kufanya makosa ya kiulinzi kama vile haileti picha nzuri. Pia tumetengeneza nafasi ambazo hatukuzitumia vizuri.

“Tutarudi kuendelea kujipanga kwa mchezo unaofuata, bado hatujakata tamaa tutahakikisha tunapambana kupata alama tatu kwenye kila mechi,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER