Pablo: Tumeazimia kushinda kila mechi

Pamoja na kujihakikishia kutinga Nusu Fainali ya Michuano ya Mapinduzi, Kocha Pablo Franco amesema tunahitaji kushinda kila mchezo.

Kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Mlandege, Kocha Pablo amesema anatarajia kufanya mabadiliko kidogo ya kikosi ili kuwalinda wachezaji.

Pablo ameongeza mechi zinachezwa karibu karibu hivyo hakuna muda wa kutosha wa maandalizi lakini mipango ni kushinda kila mchezo.

“Tumecheza jana na kesho tunacheza tena, hatukupata muda wa kujiandaa lakini tunapaswa kushinda kila mchezo.

“Tutafanya mabadiliko kidogo ya kikosi kwa ajili ya kuwalinda wachezaji. Tumeongeza wachezaji wengine kwa ajili ya majaribio ambao tutawatumia katika mashindano haya na wakituvutia tutawapendekeza kwa uongozi wasajiliwe,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER