Pablo: Tulistahili kushinda, asanteni wachezaji, mashabiki

Kocha Mkuu Pablo Franco amesema tulikuwa katika kiwango bora kwenye mchezo dhidi ya US Gendarmerie na tulistahili kupata ushindi huo mnono wa mabao 4-0 na kutinga robo fainali.

Pablo amesema kipindi cha kwanza tulitengeneza nafasi nyingi ambazo hatukuzitumia vizuri lakini kipindi cha pili tuliongeza umakini na kupata idadi hiyo ya mabao.

Pablo amewasifu wachezaji kwa jinsi walivyojituma muda wote na kuhakikisha tunatimiza malengo ya kuingia robo fainali ya michuano hii.

Raia huyo wa Hispania amewamwagia sifa mashabiki wetu walijitokeza kwa wingi uwanjani kuisapoti timu licha ya mchezo kuanza katika muda ambao haukuzoeleka.

“Tulistahili kushinda, tulikuwa bora zaidi yao. Tulitengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza lakini tulishindwa kuzitumia. Ila jambo zuri tulivyorudi tuliongeza umakini na kupata ushindi mnono.

“Niwapongeze wachezaji kwa kujitoa kwao muda wote pamoja na mashabiki ambao wamekuja kwa wingi licha ya mchezo kuanza katika muda ambao haujazoeleka,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER