Pablo: Tuko tayari kwa Orlando

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema kikosi kiko tayari kwa ajili ya mchezo wa Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Pablo amesema anaamini hali ya uwanja itakuwa faida kwetu kutokana na ruhusa tuliyopewa na Shirikisho la Soka Afrika CAF la kuujaza na tutaitumia kama faida kwetu.

Amesema anajua shauku ya Watanzania kutaka kuona timu ikitinga nusu fainali baada ya kupita miaka zaidi ya 20 ambapo sasa tuko tayari kuwapatia furaha hiyo.

“Tunacheza kwa kutafuta nafasi ya kufuzu nusu fainali siyo pointi, kwa hiyo tutahakikisha tunatumia vizuri nafasi tutakazopata ili kumaliza mchezo katika uwanja wa nyumbani.

“Kuhusu kikosi kipo tayari, tumefanya mazoezi na wachezaji wapo katika hali nzuri. Tunajua Wanatanzania wanahitaji kuiona timu ikiingia nusu fainali baada ya kupita muda mrefu nasi tutahakikisha tunafanikisha hilo.

“Hii ni mechi ya mtoano hatuhitaji pointi. Tunahitaji mtaji mkubwa wa mabao nyumbani hivyo tunapaswa kutumia nafasi tutakazopata ili kujiweka kwenye nafasi nzuri mechi ya marudiano,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER