Pablo: Hakuna timu rahisi, tutapanga kikosi Kamili

Kuelekea mchezo wa kesho wa robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Pamba FC Kocha Mkuu Pablo Franco, amesisitiza haitakuwa mechi rahisi na tutapanga kikosi kamili.

Pablo amesema ni mchezo muhimu na tunahitaji kushinda ili kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano na hatimaye tutetee taji letu.

Pablo ameongeza kuwa tutachukua tahadhari zote na hutataidharau Pamba kwakuwa ipo Championship, tumeupa umuhimu mkubwa mchezo wa kesho.

“Katika michuano hii hakuna timu rahisi, huu ni mchezo muhimu kwetu tunahitaji kushinda ili kusonga mbele. Tutapanga kikosi kamili kwa wachezaji wote walio tayari kwa mchezo.

“Nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu, tunahitaji kupata ushindi,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER